CCM KUVUNJA UKIMYA MRITHI WA KINANA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 7, 2025

CCM KUVUNJA UKIMYA MRITHI WA KINANA




Na Okuly Julius _DODOMA


Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya Mkutano wake Mkuu kuanzia Januari 18 hadi Januari 19, 2025 Jijini Dodoma ambapo ajenda kuu katika Mkutano ni tatu ambazo ni pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho kwa Serikali zote mbili Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Hayo yamebainishwa leo Januari 7,2025 Jijini Dodoma na Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama hicho CPA Amos Makalla wakati akizungumza na Waandishi wa habari.

"Mkutano huo utakuwa na agenda tatu ambapo ya kwanza ni kufanya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, agenda ya pili ni kupokea kazi za chama katika kipindi cha miaka Mwaka 2022 mpaka 2025 na agenda ya tatu ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa serikali zote mbili Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, "amesema CPA Makalla

Aidha kupitia Mkutano huo amesema watamteua Makamu Mwenyekiti wa CCM ambaye atarithi mikoba ya Abrahaman Kinana ambaye alitangaza kustaafu nafasi hiyo huku akiweka bayana namna mchakato wake utakavyokuwa mpaka upatikanaji wake.

"Kumekuwa na uvumi, unaona vichwa vya habari kwamba CCM patashika, wafuatao watajwa kurithi nafasi ya Kinana, nani kati ya hawa atachukua nafasi ya Kinana, wengine wanakwenda mbali kuandika wafuatao kuchukua nafasi ya Kinana. Kila mmoja anaandika navyotaka.

"Nataka kusema kwamba, nafasi ya Makamu Mwenyekiti haigombewi, unaposema kinyang'anyiro kinatoka wapi wakati nafasi haigombewi wala haijazwi fomu?," alieleza.

CPA Makala alisisitiza: "Tutampata makamu mwenyekiti baada ya mapendekezo ya kamati kuu na halmashauri kuu, kisha jina la atakayeziba nafasi hiyo litawasilishwa katika mkutano kuu na hapo ndipo zitapigwa kura ya ndiyo au hapana."

"Hatukuwa kimya, Chama kinaongozwa kwa katiba, kina utaratibu wake, hatuwezi kuongozwa kwa hisia za watu. Kwa sasa Kamati Kuu imeona ndiyo muda muafaka kujaza nafasi hiyo," alisema.

CPA Makalla aibainisha kuwa mkutano mkuu utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, vinavyotarajiwa kufanyika Januari 16 mwaka huu.




No comments:

Post a Comment