JAMII IMEOMBWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 27, 2025

JAMII IMEOMBWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI


Jamii imeombwa kuunga mkono juhudi za Serikali inayotekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ili kuendelea kuenzi umoja ushirikiano,amani na utulifu vilivyoasisiwa na viongozi mara baada ya uhuru wa Tanganyika.

Ushauri huo umetolewa Januari 26,2025 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Dodoma Samwel Malecela wakati wa uzinduzi wa taasisi ya NASIMAMA NA MAMA inayounga mkono juhudi za Rais Samia akisistiza mafaniko ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho.

"Kwa Maendeleo kwa Elimu,kwa umeme kwa Maji nasimama na mama amesema Malecela

Ameongeza kuwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali sio kitu kibaya suala la chama unachokuwa nacho ibaki kuwa siri yako.

"Taasisi hii nimeiona haijakaa sana kichama lakini kuwa na mlengo wa Chama si mbaya,tuwakaribishe na wenzetu ili wajue tunaongea nini hata kama ana chama chake na msimamo wake kwenye maendeleo huwa tunasimama pamoja"amesema Malecela

Mkutano huo ulitanguliwa na uchaguzi mkuu wa chama hicho baada ya kuzinduliwa rasmi taasisi hiyo.





No comments:

Post a Comment