
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji Wakili Haji Nandule, kwa niaba ya Waziri Maji amewasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa Mfuko wa Taifa wa Maji kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa kipindi cha miaka miwili ya 2022/2023, 2023/2024 na nusu ya kwanza ya mwaka 2024/2025 .
Ameainisha majukumu yanayo tekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Maji ikiwa ni pamoja na utoajiwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji katika maeneo yenye uhaba wa huduma hiyo .
Ameongeza kuwa Mfuko umekuwa ukihakiki fedha zinazopatikana kutokana na Tozo za Mafuta ya Petroli na Dizeli kwa kufuatilia taarifa za makusanyo ya tozo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kila mwezi na hivyo kuwa na taarifa sahihi ya kiasi cha fedha ambacho Mfuko unastahili kupokea kutoka Hazina.
Wakili Nandule katika taarifa yake amesema kuwa kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Desemba 2024, Mfuko wa Taifa wa Maji umetoa fedha zaidi ya Shilingi bilioni 300 zilizoelekezwa katika utekelezaji wa jumla ya miradi ya maji 785 ya usambazaji wa maji vijijini na mijini, utunzaji wa vyanzo vya maji na uimarishaji wa Maabara za Maji.
Kati ya miradi hiyo, takribani miradi 196 imekamilika na inanufaisha wananchi zaidi ya milioni tatu.
Amesema pamoja na Mfuko kuendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuongeza wigo wa mapato kupitia vyanzo mbalimbali,
Pamoja na hayo, ameweka bayana kuwa wameendelea kuzijengea uwezo taasisi katika kuandaa maandiko ya miradi yatakayowezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo.





No comments:
Post a Comment