MIRADI YA DHARURA IFANYIKE USIKU NA MCHANA:KASEKENYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 9, 2025

MIRADI YA DHARURA IFANYIKE USIKU NA MCHANA:KASEKENYA


Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amewataka wakandarasi wote Nchini waliopewa kazi za ujenzi wa miradi ya dharura kufanya kazi usiku na mchana.

Mhandisi Kasekenya, ameyasema hayo tarehe 9 Januari, 2025 Mkoani Katavi wakati akikagua miradi ya barabara na madaraja ambayo yaliathiriwa na Mvua za El-nino za mwaka 2024.

“Miradi hii ni miradi ya dharura na mwaka uliopita Mvua iliharibu sana miundombinu ya barabara hasa madaraja na Serikali ilitafuta vyanzo mbalimbali vya fedha ili kufanya marejesho ya muda na kuja kujenga madaraja ya kudumu kwa ubora unaoitajika hivyo wakandarasi mhakikishe mnafanya kazi muda wote”, amesema Mhandisi Kasekenya.

Vilevile, Mhandisi Kasekenya amewasisitiza Wakandarasi pamoja na Kitengo cha Usimamizi wa miradi cha TANROADS (TECU) kusimamia kwa karibu miradi hii kwa kufanya kazi usiku na mchana ili iweze kukamilika ndani ya muda wa miezi 12 kama ilivyopangwa kwa ubora mzuri.

Mhandisi Kasekenya amewataka TANROADS kuwawezesha wakandarasi wazawa katika kufanya kazi kwa weledi kwa sababu wameaminiwa na waoneshe nia kuwa wanaweza kufanya kazi kubwa zaidi.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende amesema kukamilika kwa madaraja hayo kutatatua changamoto za usafiri katika kipindi chote cha mwaka mzima.

Madaraja hayo ni daraja la Katuma/Sitalike, Mirumba/Kitumba pamoja na Daraja la Kilida ambayo yanajengwa kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.



No comments:

Post a Comment