
Rais mteule wa Msumbiji anaapishwa leo Jumatano huku kukiwa na hofu ya kufanyika kwa "maandamano kote nchini humo", zaidi ya miezi mitatu tangu kufanyika kwa uchaguzi uliozozaniwa.
Daniel Chapo, mwenye umri wa miaka 48, alipata asilimia 65 ya kura ambayo viongozi wa upinzani, waangalizi wa uchaguzi na wananchi kwa ujumla walisema kuwa alikuwa na dosari.
Matokeo hayo yalizua wimbi la maandamano - mengine ya amani lakini mengine ya vurugu - na kusababisha machafuko, ikiwa ni pamoja na mauaji na uharibifu.
Mpinzani mkubwa wa Chapo ni Venâncio Mondlane. Wiki iliyopita, alirejea kutoka uhamishoni alikoenda mwenyewe. Alitumia muda mwingi kuwa nchini Afrika Kusini ambako anasema alinusurika katika jaribio la mauaji.
Sasa anatoa wito kwa raia wa Msumbiji kuingia mitaani, kwa mara nyingine tena, siku ya kuapishwa kwa rais mpya "dhidi ya wezi wa watu".
No comments:
Post a Comment