TANZIA : MKUU WA WILAYA YA MBOZI AFARIKI DUNIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 14, 2025

TANZIA : MKUU WA WILAYA YA MBOZI AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. ESTER MAHAWE  enzi za uhai wake.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Hassan anasikitika kutangaza kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Ester Mahave kilichotokea leo tarehe 14.01.2025 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC mkoani Kilimanjaro alipokuwa akipatiwa matibabu.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Mhe. Ester Mahave. Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan natoa pole kwa familia, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, wafanyakazi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu huyo. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi” amesema.

Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na familia inandelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zidadi zitatolewa utakapofika wakati.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

No comments:

Post a Comment