
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP,George Katabazi amewataka wananchi wa Kijiji cha Chigongwe kuepukana na vitendo vya wizi wa mifugo katika eneo hilo ambao huleta migogoro.
Katabazi ametoa kauli hiyo Januari 28,2025 wakatiki akifanya ziara ya katika kata ya chigongwe na kuzungumza na wananchi na wafanyabiashara ya mifugo katika kata hiyo
Aidha Katabazi amesema Jeshi la Polisi tayari linawashikilia watuhumiwa wa wizi wa mifugo katika Kijiji hicho ambapo amesema tayari mtandao wa wizi huo, wanaoshirikiana na baadhi wafanya biashara ya nyama umebainika na watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria
Vile vile katabazi amewasihi wananchi hao kuweka mazizi salama pamoja na kuwa na utaratibu wa kuhoji vibali, pindi wanapoona mifugo inaswagwa kiholela na kushirisha uongozi wa Kijiji na Jeshi la Polisi ili kudhibiti wizi huo.
Ziara ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ya kutembelea kata zote zilizopo katika Jiji hili inalengo la kusikiliza kero za wananchi,utatuzi wa migogoro pamoja na kutoa elimu ya ulinzi na usalama kwa wananchi.






No comments:
Post a Comment