Na Carlos Claudio, Dodoma.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) katika Operesheni ya ukusanyaji wa Madeni kwa wateja wenye Madeni Sugu na ukaguzi wa Miundombinu imebaini uwepo wa Mteja aliyechepusha maji (kuiba Maji) kwa kufungua plagi na kuunganisha bomba kwa kufunga mpira akitumia maji bila kupita katika mita.
Akizungumza mara baada ya Operesheni ya leo Februari 19, 2025 iliyofanyika katika Mtaa wa Kisasa Daraja Dogo Afisa Mapato (DUWASA) KHALIFA ISMAILY IBRAHIM amesema mteja huyo alikatiwa maji kwa kipindi cha miezi 3 kwa kudaiwa shilingi laki 6 na elfu 55.
“Tupo katika oparesheni zetu za kawaida kwa wateja ambao wamesitishiwa huduma za maji katika jiji la Dodoma na tumefika kwa huyu mteja Cornel Tarimo kwaio tukaona tuje kukagua tuangalie tatizo nini, lakini kama unavyoona tumemkatia kwa kifaa kinachoitwa plagi na alichokifanya amefungua plagi alafu ameunganisha bomba amefunga na mpira na maji yamapita moja kwa moja yanatumika bila kupita kwenye mita”,
“Hiki kitendo siyo kizuri kwasababu kikubwa ninachosema waje DUWASA tuweze kuzungumza nao tuwape njia rahisi ya wao kuweza kulipa fedha hizi na kuweza kurejesha huduma ya maji na waweze kutumia maji kwa uhalali”, ameeleza Afisa Mapato kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma DUWASA Ibrahim.
Amesema kitendo cha wateja kujiunganishia maji kinyemela ina athari kubwa kwa nchi kwani kitendo hicho ni kuhujumu uchumi hivyo ametoa onyo kwa wana Dodoma na nchi nzima wanaoendelea na kitendo hicho cha uchepushaji wa maji.
Kwa upande wake Zaina Omari mfanyakazi wa kituo cha mafuta (sheli) ya Dubai Energies amesema mita hiyo inatumika na watu watatu ikiwemo kituo cha mafuta (sheli) ya Dubai Energies, kituo cha kuoshea magari na wapangaji wawili.
“Aliyeunganisha maji haya kinyemela mimi simjui na kitendo hiki kilichofanywa siyo kizuri hivyo natoa wito wa wateja wa DUWASA wasifanye vitendo kama hivi,” amesema Zaina.
No comments:
Post a Comment