ANWANI ZA MAKAZI KUCHOCHEA UKUAJI WA UCHUMI-MAJALIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 8, 2025

ANWANI ZA MAKAZI KUCHOCHEA UKUAJI WA UCHUMI-MAJALIWA

 


Na Carlos Claudio,Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza wizara ya mawasiliano na Teknolojia ya habari kuhakikisha inakamilisha maandalizi ya sheria ya matumizi ya anwani za makazi ili kuweka masharti ya msingi ya matumizi ya mfumo wa NaPA.


Majaliwa amesema hayo leo Januari 8,2025 jiji Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) wakati akihitimisha kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya anwani za Makazi ambapo amesema mfumo wa anwani za makazi unakwenda kulinda na kukuza uchumi wa kidigitali.


Amesema oparesheni ya mfumo wa anwani za makazi nchini umewezesha ukusanyaji wa taarifa milioni 12.3 za anwani za makazi ambazo zimehifadhiwa katika mfumo wa kidijitali unaojulikana kwa jina la National Physical Addressing (NaPA).


“siku kama ya leo tarehe 8 Februari, 2022, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizindua utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi nchini kwa njia ya operesheni. Operesheni hiyo ilifanyika kwa muda wa miezi minne na kuwezesha ukusanyaji wa taarifa milioni 12.3 za anwani za makazi zilizohifadhiwa katika mfumo wa kidijitali wa anwani za makazi unaojulikana kwa jina la National Physical Addressing (NaPA),”


“Hii ni programu bora na inarahisisha kupata huduma husika sambamba na kwenda na kasi ya kimaendeleo katika uchumi wa sasa wa Kijiditali, vibao tulivyoviweka kuonesha mitaa na barabara, tunao Watanzania ambao si waaminifu wanang’oa mabago hayo na kwenda kuyauza, ni muhimu kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hiyo kwa sababu inamanufaa, amesema Majaliwa”.



Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema kuwa Wizara yake imeandaa Mpango wa mkakati kwa waratibua wa kuhakikisha wamepatiwa vishikwambi kwajili ya kuimarisha utekelezaji na uendelezwaji wa mfumo wa anwani za makazi.


Amesema kuwa amesema Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaendelea kusimamia na kuendeleza miundombinu na mifumo ya msingi (Foundation Systems), ambayo ni mhimili muhimu wa uchumi wa kidijitali ulioainishwa katika Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali wa Miaka 10 (2024–2034).


“Tunatambua kwamba miji yetu inaendelea kukua kila kukicha, watu wetu wanahama kutoka eneo moja kwenda lingine na teknolojia zinabadilika. Wizara kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI tumejipanga kuhakikisha Mfumo huu unakuwa endelevu,”


“Tutaendelea kufanya uhakiki wa taarifa, Kujenga uwezo kwa watendaji wetu wa serikali za mitaa ili waendelee kuhuisha taarifa, kutunga sheria ya anwani za makazi, kuboresha mfumo wa kidijitali wa NaPA na kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi.” amesema Silaa.


Naye Naibu Waziri,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Festo Dugange amesema kuwa kupitia mfumo huo  umewarahisishia utoaji huduma za Kijamii ikiwemo usambazaji wa Madawa kwenye vituo vya afya huku Naibu Waziri wa Mawasiliano na uchukuzi wa Zanzibar,Nabil Abdulatif Awadhi amesema kuwa zoezi la anwani za makazi Zanzibar limekamilika kwa asilimia100.









No comments:

Post a Comment