BODI YA AQRB YAIMARISHA UWAJIBIKAJI NA UKUSANYAJI MAPATO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 10, 2025

BODI YA AQRB YAIMARISHA UWAJIBIKAJI NA UKUSANYAJI MAPATO




Na Okuly Julius _DODOMA


BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI (AQRB) imetakiwa kuhakikisha wanawafuatiliwa Watumishi wa Bodi ambao wanamiliki Kampuni zinazofanya Kazi za Kitaaluma kuepuka utovu wa nidhamu unaoweza kutokea ikiwemo mgongano wa maslahi.

Kauli hiyo imetolewa leo Februari 10 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa AQRB, Mbunifu Majengo Dkt. Ludigija Boniface Bulamile, wakati akifungua MKUTANO WA KUMI NA MOJA WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI.

Amesema kuwa Bodi ya Wakurugenzi inathamini mchango wa Menejimenti na kwamba inahitaji michango yao zaidi katika kuwezesha kuendelea na ujenzi wa Tasnia za Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi.

"Bodi ya Wakurugenzi inawataka watumishi wa bodi hiyo kujijengea uwezo kupata uzoefu, ujuzi na hatimaye kushindana Kitaifa na Kimataifa.,"

Na kuongeza kuwa "Mkutano huu ni jukwaa muhimu la kuwashirikisha Watumishi katika kufikia maamuzi yanayohusu kuiendeleza Bodi," amesema

Kwa upande wake, Msajili wa Bodi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Mbunifu Majengo Edwin Nnunduma amesema kuwa Bodi imeongeza makusanyo ya mapato kwenye miradi iliyosajiliwa kutoka Sh bilioni 2.2 hadi kufikia bilioni 5.9

"Idadi ya usajili wa Wataalam imeongezeaka kutoka 75 hadi- 279 na Kampuni imeongezeka kutoka 19 – 53. Miradi iliyokaguliwa imekuwa ikiongezeka lakini kikubwa ni ongezeko la makusanyo ya mapato kwenye miradi iliyosajiliwa kutoka bilioni 2.2 hadi bilioni 5. 9, "amesema

Amesema kuwa bodi imekuwa ikifanya vizuri katika ukusanyaji wa madeni (ada za mwaka) kutoka kwa wataalamu na makampuni yaliyosajiliwa.

"Bodi imekuwa ikiimarisha uwajibikaji na uwazi katika Kukusanya Mapato na Matumizi ya Fedha takriban katika shughuli zote zinazofanywa na Bodi," amesema

Amesema kuwa ripoti ya CAG kwa mwaka 2023/2024, imeipongeza Bodi kwa mifumo ya udhibiti wa vihatarishi na udhibiti wa ndani, ikisema Bodi ilitathmini mifumo ya udhibiti wa ndani katika mwaka mzima wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2024 na ina maoni kwamba Bodi ilifanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Amesema kuwa mkutano huo utapokea taarifa ya Mpango na Bajeti ya Bodi kwa mwaka wa fedha 2025/2026, kuwasilisha na kuzipatia majibu hoja za Watumishi zitakazowasilishwa na TAMICO.

"Bodi baada ya uchambuzi wa kina imepitisha vipaumbele ambavyo inaviona ni vya muhimu zaidi na vinaweza kutekelezeka kwa mwaka wa fedha 2025/26 ikiwemo ukuaji wa Miundombinu na TEHAMA na kukuza Sekta ya Fedha," amesema

Amesema kuwa kutokuwa na uwezo wa kukusanya mapato ya kutosha kwa ajili ya shughuli zake. Msingi wa mapato bado unategemea ufadhili wa Serikali ingawa juhudi za kupunguza utegemezi huo kupitia vyanzo vyake zinaendelea.

"Bodi haijaweza kuongeza idadi ya Wataalamu waliosajiliwa ili kufikia Wataalam 5,000 waliopo kwenye Mpango Mkakati," alisema

Pia Bodi haijaweza kutumia uwezo kamili katika ukaguzi wa miradi iliyo katika kanda zilizo na viwango vikubwa vya ujenzi kwa sababu ya uhaba wa Wafanyakazi na Vitendea kazi.

"Bodi haijaweza kutunza,kukarabati ofisi zake za makao makuu na kanda ili kuongeza taswira nzuri kwa Wateja. Bodi haijaweza kujenga jengo la Makao Makuu linalofaa na kutoa nafasi kwa madhumuni ya uwekezaji.," amesema

Baraza la Wafanyakazi unafanyika kwa mujibu wa Ibara Na. 7 na Na. 20 ya Agizo la Rais Na. 1 la mwaka 1970 ikisomwa pamoja na Kifungu Na. 73(1) - (3) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004 na Kanuni Na. 108 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.






No comments:

Post a Comment