
Na Saida Issa,Dodoma
Serikali imeshauriwa kuimarisha mfumo wa kodi ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kuchochea ukuaji wa Pato la Taifa.
Akiwasilisha taarifa ya mwaka kuhusu utekelezaji wa majukumu ya kamati ya Bunge ya Bajeti kwa kipindi cha februari 2024 hadi january 2025 mwenyekiti wa kamati hiyo Oran Manase Njeza amesema kumekuwepo na changamoto katika utekelezaji wa sera za kodi, hususan mabadiliko ya mara kwa mara katika usimamizi wa kodi ya majengo kati ya TRA na Serikali za Mitaa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2024, Serikali ilikusanya asilimia 51.9 ya bajeti yake, ikionyesha mwenendo mzuri wa mapato.
Hata hivyo, Kamati imesisitiza kuwa kuna haja ya kuwa na sera thabiti za kodi ili kuongeza ufanisi wa makusanyo na kuhakikisha vyanzo vya mapato vinadumu kwa muda mrefu.
Amesema Kutokuwepo kwa uthabiti katika sera za kodi, hususan mabadiliko ya mara kwa mara kwenye usimamizi wa kodi ya majengo kati ya TRA na Serikali za Mitaa, kumekuwa na athari katika ufanisi wa makusanyo.
Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2024, Serikali ilikusanya asilimia 51.9 ya bajeti yake, ikionyesha mwenendo mzuri wa mapato
Kuhusu uchumi wa Tanzania Njeza amesema Uchumi unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024 na kufikia asilimia 6.0 mwaka 2025, kutokana na uwekezaji katika miradi ya maendeleo na uboreshaji wa mazingira ya biashara.
Kamati imependekeza kuwa, ili kufanikisha ukuaji huo, Serikali inapaswa kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, na kuhakikisha mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato inatumika ipasavyo.
Serikali pia imehimizwa kuimarisha ushirikiano na washirika wa maendeleo ili kupata fedha zaidi kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ambayo ina mchango mkubwa katika kuongeza mapato na kuboresha uchumi wa nchi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment