Na Okuly Julius _DODOMA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emanuel Nchimbi amewataka Makatibu wa Matawi wa Chama hicho kutenda haki, kutopuuza Katiba na kujiepusha na masuala ya RUSHWA wakati Chama kikielekea kwenye uchaguzi Mkuu 2025.
Balozi Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Februari 19,2025 jijini Dodoma wakati akifungua Habari ya jioni wapendwa,
Kesho Februari 19,2025 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa Watendaji wa Kata na Makatibu Tawi wa Chama hicho kwa Mkoa wa Dodoma
Amesema katika siku za hivi karibuni kumezuka utaratibu kwa baadhi ya makada wa CCM kutengeneza matukio ya kumbukizi za kuzaliwa,kumbikizi za ndoa na kuwaalika wanachama na kuwalipa posho.
"Niseme wazi chama Cha Mapinduzi CCM kina mfumo wake wa kufuatilia kila kinachotokea na kumbukumbu hizi tunazokusanya ndizo zitakazowaengua au kuwatoa kwenye kugombea, " Amesema Dkt Nchimbi
Aidha akielezea mafunzo hayo amesema
ni maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kuwa na watendaji wanaotambua wajibu wao .
" Mafunzo haya yanakwenda kuwakumbusha majukumu yenu kama watendaji wa chama na jinsi gani tutashinda kwa kishindo uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, " Amesema
Na kuongeza " Hii iko wazi lengo kuu la chama chochote cha siasi ni kushika dola hivyo kwa upande wetu dola tumeshika kikubwa ni kushinda kwa kishindo kwani kushindwa kwa chama kunatokana na wanachama husika na kushinda kwa chama kunategemea wanachama hivyo tukawe waadilifu, " Amesema
Kwa upande wake Katibu NEC Organization Issa Haji Gavu amesema mafunzo hayo ni maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kusimamiwa na Katibu Mkuu Dkt Nchimbi.
" Kwanini mafunzo haya kwa watendaji hawa ni kwasababu chama kipo na kinaanzia kwenye ngazi ya Shina hadi Taifa hivyo niwaombe muwe wasikivu na kuzingatia mnavyoelekezwa, " Amesema Gavu.
Naye Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga amesema mafunzo hayo kwa watendaji wa Kata na Matawi yanakwenda kuwajenga kwani wapo nyuma ya muda na mafunzo haya yataleta muongozo .
No comments:
Post a Comment