
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imetunukiwa TUZO ya Matumizi Bora na Sahihi ya Mifumo ya TEHAMA katika Utoaji wa Huduma kwa Wananchi kwa kushinda nafasi ya Tatu.
DUWASA imetangazwa mshindi wa Tatu kati ya Taasisi zote za Umma nchini katika Mkutano wa Tano wa Serikali Mtandao (e-Government) uliyofanyika Jijini Arusha kuanzia Februari 11 - 14, 2025.

No comments:
Post a Comment