KATIMBA: SERIKALI IMEENDELEA KUCHUKUA HATUA KUPUNGUZA UHABA WA WALIMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 22, 2025

KATIMBA: SERIKALI IMEENDELEA KUCHUKUA HATUA KUPUNGUZA UHABA WA WALIMU


OR-TAMISEMI


Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba, amesema serikali inaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na upungufu wa walimu kwa kuajiri kila mwaka kulingana na upatikanaji wa fedha, huku kwa sasa ikiwa katika majaribio ya matumizi ya teknolojia ya madarasa janja.

Mhe. Katimba ameyasema hayo leo, Februari 22, 2025, alipokuwa akizungumza na Maofisa Elimu Kata waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya matumizi ya Madarasa Janja katika Taasisi ya Elimu Kibaha, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuajiri walimu kila mwaka kwa kutoa vibali vya ajira, huku ikiimarisha utaratibu wa kuwatumia walimu wa kujitolea.

"Watanzania wamehamasika kupeleka watoto shule, na udahili wa wanafunzi umeongezeka maradufu, hali iliyosababisha upungufu wa walimu. Hivyo, serikali, pamoja na kuajiri, imebuni teknolojia ya kutumia madarasa janja, na kwa sasa ipo katika hatua za majaribio," amesema.

Pia, Mhe. Katimba amebainisha kuwa pamoja na jitihada hizo, serikali inaendelea kupandisha madaraja ya walimu kama sehemu ya motisha ya kiutendaji.

No comments:

Post a Comment