KILWA YARINDIMA SIKU YA WAPENDANAO DUNIANI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 14, 2025

KILWA YARINDIMA SIKU YA WAPENDANAO DUNIANI.

 

📍Ni mwendo wa Shamrashara za watalii ndani ya TAWA SEA CRUISER

Siku adhimu Kwa ajili ya kuwakutanisha wapendanao almaarufu Valentine's Day inaendelea vyema ndani ya Hifadhi ya urithi wa utamaduni wa dunia ya Magofu ya Kale ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ambapo watalii kutoka sehemu mbalimbali wapo ndani ya Hifadhi hiyo wakisheherekea Kwa kubarizi ndani ya boti la kisasa lijulikanalo Kwa jina la TAWA SEA CRUISER

Kadri muda unavyosonga ndivyo Idadi ya watalii inavyozidi kuongezeka kwa Kasi na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kupitia Hifadhi hiyo inatarajia kupokea wageni wengi siku ya leo kutokana na mvuto wa Hifadhi hiyo ambayo hivi karibuni imekuwa ikipokea Idadi kubwa ya watalii kutoka Mataifa mbalimbali duniani na watalii wa ndani.

TAWA inaendelea kuwakaribisha watu wote kutembelea hifadhi hiyo kujionea vivutio vya kihistoria na kiutamaduni ikiwemo kufurahia mandhari nzuri za fukwe pamoja kuona viumbe vya majini kupitia TAWA SEA CRUISER.

No comments:

Post a Comment