Na Okuly Julius – Dodoma
Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imechukua hatua kadhaa kuhakikisha wakandarasi wazawa wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu nchini.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi cha miaka minne ndani ya sekta ya ujenzi leo Februari 17,2025 jijini Dodoma , Mkurugenzi wa Mipango ya Miundombinu wa TANROADS, Mhandisi Ephatar Mlavi, amesema hatua hizo zimechukuliwa kufuatia changamoto ya ushiriki hafifu wa wakandarasi wa ndani katika zabuni na miradi inayotekelezwa.
Mikakati ya Kuimarisha Ushiriki wa Wakandarasi Wazawa
Mhandisi Mlavi amesema kuwa miongoni mwa mikakati iliyopendekezwa ni:
🎈🎈Kutenga 10% ya bajeti ya kila mwaka ya maendeleo kwa miradi ya mafunzo kwa vitendo.
🎈🎈Kutenga angalau 30% ya bajeti ya maendeleo kwa ajili ya upendeleo kwa wakandarasi wazawa.
Kutenga angalau 5% ya bajeti ya miradi ya maendeleo kwa makundi maalum.
Aidha, TANROADS inaendelea kufuata sheria na kanuni za ununuzi ambazo zimeongeza fursa kwa wakandarasi wazawa kushiriki katika zabuni zinazotangazwa kitaifa, ikiwa ni pamoja na miradi yenye thamani ya hadi TZS 50,000,000.00.
Mhandisi Mlavi ameongeza kuwa miradi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina inayotumia fedha za ndani inapaswa kutekelezwa na makampuni ya washauri elekezi wazawa. Kwa miradi inayotumia fedha za mikopo na misaada, inapendekezwa kutekelezwa kwa ushirikiano kati ya washauri elekezi wazawa na wale wa nje.
"Ili kuhakikisha wazabuni wa ndani wananufaika na zabuni za ushauri elekezi, TANROADS inahimiza ushirikiano kati ya makampuni ya ndani na yale ya nje. Jitihada hizi zinatarajiwa kuongeza ujuzi, uzoefu, na uwezo wa wakandarasi wa ndani katika sekta ya ujenzi wa barabara na miundombinu mingine muhimu," amesema Mhandisi Mlavi.
Pia, amesema TANROADS imetoa nafasi za ushiriki wa mafunzo kwa wanafunzi na wahitimu 1,500 wa fani za uhandisi katika miradi inayotekelezwa, huku kazi za matengenezo ya barabara na madaraja zikitekelezwa na wakandarasi wazawa na kusimamiwa na washauri elekezi wazawa pekee.
Maendeleo ya Miradi ya Barabara Nchini
🎈🎈Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 15,625.55 zimekuwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kati ya hizo:
🎈🎈Kilometa 1,365.87 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Kilometa 2,031.11 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.
🎈🎈Kilometa 2,052.94 na madaraja mawili yamefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, huku serikali ikiendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wake.
"Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inasimamia ujenzi, ukarabati, na matengenezo ya barabara na madaraja kwenye mtandao wa barabara wenye urefu wa jumla ya kilometa 37,435.72. Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara zenye jumla ya kilometa 4,734.43 na madaraja kumi unaendelea," amesema Mhandisi Mlavi.
Aidha, TANROADS ina miradi ya barabara yenye urefu wa takriban kilometa 5,326.90 na miradi saba ya madaraja ambayo ipo katika hatua ya manunuzi kwa ajili ya kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara hizo kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, ametoa wito kwa vyombo vya habari kutumia fursa ya mikutano hiyo kuwapa wananchi taarifa za miradi na shughuli mbalimbali zilizotekelezwa na serikali katika kipindi cha miaka minne.
Pia, amewasisitiza viongozi wa taasisi za umma kuja kutoa taarifa za utendaji wa taasisi zao ndani ya kipindi hicho na kwa wale ambao hawatatekeleza agizo hilo watatakiwa kueleza sababu za kutofanya hivyo.

No comments:
Post a Comment