Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu wanane wakituhumiwa kuhusika katika matukio mawili tofauti likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi katika wilaya ya Chemba mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari February,10,2025 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), George Katabazi amesema kuwa wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao kufuatia operesheni maalum inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani hapo.
Katika tukio jingine Kamanda Katabazi amebainisha kuwa wamemkamata Juma Hamza maarufu jambazi mwenye umri wa miaka 27 akiwa na watuhumiwa wenzake sita vijana wenye umri kati ya miaka 20 na 30 ambao wana mtandao uitwao Maronjo kwa tuhuma za kujeruhi watu watatu na kuhusika na matukio ya wizi,ubakaji na unyang'anyi wa kutumia silaha.
Sambamba na hilo Katabazi ametoa onyo kali kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwamba Jeshi la polisi mkoani humo halitowaonea muhali.
No comments:
Post a Comment