OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAPATIWA ELIMU YA KINGA NA TAHADHARI DHIDI YA MAJANGA YA MOTO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, February 4, 2025

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAPATIWA ELIMU YA KINGA NA TAHADHARI DHIDI YA MAJANGA YA MOTO



Na. Mwandishi Wetu


Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wameaswa kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto pamoja na matumizi sahihi ya namba ya dharula 114 ili kutunza jengo la ofisi hiyo na kuendelea kutoa huduma kwa wateja wanaofika ofisini hapo bila kuwa na shaka yoyote.

Wito huo umetolewa na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Bw. Iddi Chanyika wakati wa mafunzo kwa watumishi wa ofisi hiyo yanayotolewa kila Jumatatu ya wiki kwa lengo la kujenga uelewa wa masuala ya kiutumishi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Bw. Chanyika ameeleza kuwa, Ofisi ya Rais-UTUMISHI inapokea wateja wengi kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, ili kulinda usalama wa wateja wanaoingia na kutoka kwa ajili ya kupata huduma hizo ni muhimu kuchukua tahadhari hasa katika kuangalia usalama wa jengo la ofisi hiyo.

Aidha Bw. Chanyika ameipongeza Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kuwa na vifaa mbalimbali vya tahadhari kwa ajili ya kujikinga na madhara ya moto yanayoweza kutokea.

“Niipongeze ofisi hii kwa kuzingatia usalama wa jengo kwani nimeona mna vifaa kwa ajili ya tahadhari dhidi ya moto vikiwemo ving’amua moto,’’ amesema Bw. Chanyika

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji ametoa shukrani kwa niaba ya Watumishi wa ofisi hiyo kwa mafunzo mazuri ambayo yatasaidia kuongeza umakini katika utunzaji wa majengo ya ofisi hiyo na kuahidi kuchukua tahadhari zote zinazohusu kinga dhidi ya majanga ya moto.






No comments:

Post a Comment