SERIKALI YATOA UFAFANUZI ASILIMIA 20 YA KODI YA ARDHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 10, 2025

SERIKALI YATOA UFAFANUZI ASILIMIA 20 YA KODI YA ARDHI


Na Josephine Majura, WF – Dodoma


Serikali imesema kuwa asilimia 20 ya mapato ya kodi zitarejeshwa katika halmashauri husika baada ya Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuhusu kuboresha usimamizi na ukusanyaji wa kodi hiyo utakapo kamilika.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hassan Seleman Mtenga wakati ambao Serikali itarejesha makusanyo ya Kodi ya Ardhi ya asilimia 20 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Mhe. Dkt. Nchemba alisema Serikali kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2023/24 ilifanya marekebisho ya Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura 290 kwa kuzitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuingia Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) katika usimamizi na ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi na kuweka utaratibu wa urejeshaji wa asilimia 20 ya mapato kwa halmashauri ili kuziwezesha katika ufuatiliaji na ukusanyaji wa mapato hayo.

"Serikali iliweka utaratibu huo ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa kuna tija katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na pango la ardhi inaongezeka na kuondoa kero zilizokuwa zinawakabili walipa kodi kwenye maeneo husika", alibanisha Dkt. Nchemba.

Alilihakikishia Bunge kuwa Mkataba huo utakapokamilika na kuwasilishwa Wizara ya Fedha, fedha hizo zitarejeshwa kama utaratibu unavyotaka.


Mwisho.





CAPTIONS

 

 1.CR2
 2.CR2
 3.JPG
 4.CR2
1.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hassan Seleman Mtenga , bungeni jijini Dodoma.

 

 2.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akichangia hoja kuhusu Taarifa ya Mwaka ya Kamati ya Bajeti kuhusu Utekelezaji wa Majukumu katika kipindi cha Februari, 2024 hadi Januari, 2025, tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa Kipindi cha nusu mwaka, Julai hadi Desemba, 2024 pamoja na Taarifa ya Mwaka ya Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma ya Mwaka 2024/2025, bungeni jijini Dodoma.

 

3. 

Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha wakifuatilia shughuli za Bunge jijini Dodoma. Kutoka juu ni Kamisha wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. Chotto Sendo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Dennis Simba na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Daniel Masolwa.

 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF - Dodoma)

No comments:

Post a Comment