TANZANIA YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA MASHINDANO YA UANDISHI WA INSHA YA EAC NA SADC - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 10, 2025

TANZANIA YAENDELEA KUNG’ARA KATIKA MASHINDANO YA UANDISHI WA INSHA YA EAC NA SADC


Na Okuly Julius - DODOMA


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa tuzo kwa wanafunzi washindi wa mashindano ya uandishi wa insha kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2022, huku Tanzania ikiendelea kung’ara kwa kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya EAC kwa mwaka wa sita mfululizo.

Katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara hiyo, Petro Makuru, aliyemwakilisha Katibu Mkuu, alisema kuwa mashindano hayo yanawajengea wanafunzi uelewa mpana kuhusu jumuiya hizo na kuwaandaa kuwa waandishi mahiri wa siku zijazo.

Bw. Makuru, amesema kuwa uandishi wa insha ni sehemu ya mafunzo na inawajengea wigo mpana wa kujifunza masuala muhimu yanayohusu jumuiya hizo.

"Mashindano hayo ni sehemu ya mkakati mkubwa wa EAC na SADC katika kujenga uelewa wa wanafunzi kuhusu kazi na mipango ya jumuiya na kwamba ni muhimu kuwahamasisha wakashiriki kwa wingi."amesema Bw. Makuru

Aidha amesema uandishi ni sanaa na ni muhimu kwasasa kuwa na utaalamu huo nchini kwa kuwa wanatengenezwa kuwa waandishi wa vitabu vya Tanzania.

Hata hivyo ametoa wito kwa wazazi na walimu kuhamasisha wanafunzi kushiriki mashindano hayo kwa kuwa yanawaandaa vyema kwenye mitihani yao ya mwisho na kuwajenga kwenye umahiri wa kuandika vitabu.

Awali, Mratibu wa mashindano ya Mashindano ya Uandshi wa Insha kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Matuha Salum Massati.ametoa wito kwa walimu na wazazi kuwahimiza wanafunzi kushiriki katika mashindano hayo na mengine kutokana na uzoefu kuonesha washiriki hufanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho ya kuhitimu kidato cha nne na sita.

'Mashindano hayo husimamiwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) kwa insha za nchi za Afrika Mashariki (EAC) na za SADC husimamiwa na Wizara ya Elimu kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar."amesema

Aidha amesema kuwa wanafunzi 1,221 walishiriki mashindano hayo kwa mwaka 2022 na baada ya usahihishaji wamepatikana washindi 20 ngazi ya taifa ambao wote watapewa zawadi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na tathmini kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Petro Makuru,akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi ambao ni washindi wa uandishi wa insha kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2022,kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,jijini Dodoma.

Mratibu wa mashindano ya Mashindano ya Uandshi wa Insha kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Mwalimu Matuha Salum Massati ,akielezea utoaji wa tuzo hizo washindi wa uandishi wa insha kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2022,hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Washindi wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na tathmini kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Petro Makuru (hayupo pichani),wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa uandishi wa insha kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2022,jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na tathmini kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Petro Makuru,akiwakabidhi tuzo wanafunzi ambao ni washindi wa uandishi wa insha kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2022,kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment