RPC,KATABAZI UHALIFU UMEPUNGUA DODOMA KUPITIA MICHEZO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, February 10, 2025

RPC,KATABAZI UHALIFU UMEPUNGUA DODOMA KUPITIA MICHEZO


Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP),George Katabazi amewataka wananchi wa kata ya Nzuguni kushiriki katika michezo mbalimbali na kuepukana na makundi ya uhalifu.

Katabazi ameyasema hayo February,8,2025 wakatika akifunga ligi ya mpira wa miguu katika kata ya Nzuguni na kutoa zawadi Kwa washindi walio ibuka kidedea katika ligi hiyo ya Rpc Katabaz Cup.

Vilevile Katabazi amesema kupitia dhana ya Polisi Jamii ya michezo uhalifu umepungua Kwa kiasi kikubwa katika Jiji la Dodoma kwani vijana wamekuwa wajitokeza Kwa wingi kushiriki katika michezo na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao.

Katika fainali hiyo timu ya Bodaboda Fc imeibuka mshindi dhidi ya Nzuguni Rangers Fc baada ya kuchuana vikali mpaka hatua ya mikwaju ya penati na kukabidhiwa kombe pamoja na zawadi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment