Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) Bi. Roselyne Massam, leo amekabidhi rasmi Sera ya Michezo kwa Wafanyakazi “Sports for the Well-Being of Workers” kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha yenye lengo la kuimarisha sekta hiyo kwa wanachama wake kote nchini.
Bi. Massam amesema, hatua hiyo inalenga kuongeza ushirikiano kati ya BMT na SHIMMUTA katika kukuza na kuratibu michezo mahala pa kazi kwa wanachama wa shirikisho hilo na kuimarisha ustawi wa wafanyakazi kupitia michezo kama nyenzo ya afya, mshikamano, kuongeza tija kazini pamoja na kuongeza ajira hivyo kuchochea maendeleo nchini.
Akipokea Sera hiyo, Bi. Msitha amewapongeza SHIMMUTA kwa hatua hiyo nzuri na kuongeza kuwa BMT ndiyo Taasisi ya Serikali yenye dhamana ya kusimamia sekta ya michezo nchini iliyoundwa kwa mujibu wa sheria namba 12 ya mwaka 1967 sura ya 49, hivyo ni wajibu wake kuhakikisha michezo yote inatekelezwa kwa kuzingatia Miongozo, Kanuni na Sheria za Michezo nchini.



No comments:
Post a Comment