TARURA YAENDELEA KUONDOA VIKWAZO KATIKA BARABARA WILAYANI KAKONKO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, February 19, 2025

TARURA YAENDELEA KUONDOA VIKWAZO KATIKA BARABARA WILAYANI KAKONKO


Kakonko, Kigoma


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara za wilaya kupitia mradi wa RISE sehemu ya uondoaji vikwazo katika barabara hususani maeneo ya vijijini.

Meneja wa TARURA wilaya ya Kakonko Mhandisi John Ambrose amesema, kwa mwaka wa fedha 2023/24 wilaya ya Kakonko ilipata fedha kwa ajili ya mradi wa uondoaji vikwazo katika barabara ya Nyabibuye-Rumashi-Kabare yenye urefu wa Km 21 iliyopo kijiji cha Kabare kata ya Gwarama, Halmashauri ya Kankonko mkoani Kigoma ambapo mradi umejenga mifereji ya maji ya mvua Km 1.3, makalavati 4 na vivuko vya waenda kwa miguu.

“Kabla ya ujenzi kulikuwa na kero iliyosababisha matengenezo ya mara kwa mara kutokana na maji yaliyosababisha kuwa na korongo kubwa lililokuwa linaleta madhara kwa wananchi wakati wa mvua, lakini sasa tumeweza kuitatua kero hii na wananchi wanasafiri bila shida, mradi umakamilika kwa 100% na upo katika kipindi cha matazamio”, amesema.

Naye, Mhe. Fidel Nderego Diwani wa kata ya Gwarama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kakonko amesema, hapo awali kulikuwa na korongo lililoleta madhara makubwa kwa wananchi pamoja na mifugo hivyo wameishukuru serikali baada ya kutoa fedha TARURA ilifanya kazi usiku na mchana ili kuondoa kero hiyo.

Naye, mkazi wa kijiji cha Kabare, Bi. Nesta Kizoya ameishukuru serikali kwa kuwatatulia changamoto hiyo kwani watoto wao walikuwa wanasumbuka kwenda shuleni pia walikuwa wanahangaika kutembelea ndugu na jamaa, lakini sasahivi wanawashukuru viongozi wao wanasafiri bila shida na kufika mashambani.

Kwa upande wake, Bi. Immaculata Magiro mkazi wa kijiji cha Kabare amesema, mvua ikinyesha ilikuwa shida watu walikufa kwasababu ya maji mengi sasahvi wanashukuru hawapati shida tena ya maji kuingia majumbani kwao pia wanaiomba serikali wawamalizie kipande kinachobaki.

No comments:

Post a Comment