TIC YAONGEZA FURSA ZA UWEKEZAJI KWA WATANZANIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 27, 2025

TIC YAONGEZA FURSA ZA UWEKEZAJI KWA WATANZANIA



Na Okuly Julius ,Dodoma


Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC) imesema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita imeweza kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa mtanzania ambapo imepunguza kiwango cha uwekezaji kutoka Dola za kimarekani laki 1 hadi Dola 50, 000.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Bw. Gilead Teri, wakati akizingumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita leo tarehe 27 Februari, 2025, katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.

"Lengo la kupunguza kiwango cha uwekezaji kwa mtanzania kutoka dola laki 1 hadi 50000 ni kutoa fulsa kwa watanzania wengi zaidi kujitokeza kuwekeza kwenye nchi yao.hilo ni moja ya jambo kubwa ambalo Rais, Samia Suluhu Hassan amefanya sambamba na kufanya mabadiliko ya sheria ya uwekezaji ikiwa ni miaka 20 baadaye tangu kuanzishwa kwa kitio hicho mwaka 1991"amesema Teri.

Amesema Katika kipindi cha Awamu ya Sita, kuanzia Januari 2021 hadi Januari 2025, TIC imesajili miradi 2,020, ambayo ni ongezeko la asilimia 91 ikilinganishwa na miradi 1,057 iliyosajiliwa katika kipindi cha 2017-2020.

Amesema thamani ya mitaji ya miradi hiyo inakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 23.67, ikiongezeka kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2.

Aidha, miradi hiyo inatarajiwa kutoa ajira 523,891, ongezeko la asilimia 284.6 ukilinganisha na ajira 136,232 za 2017-2020.
Katika miradi hii, asilimia 34.3 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya wageni, na asilimia 23.1 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni.

Katika hatua nyingine Bw. Teri amesema tathmini inaonesha kuwa idadi kubwa ya miradi iliyosajiliwa ipo katika sekta za kipaumbele ambapo Sekta ya uzalishaji viwandani inaongoza kwa kuwa na jumla ya miradi 917 sawa sawa na asilimia 45.39 ikifuatiwa na Sekta ya Usafirishaji yenye miradi 348 sawa na asilimia 17.22 na kufuatiwa na Sekta ya Ujenzi wa majengo ya biashara 304 sawa asilimia 15.04.

Sekta ya nne inayoongoza kufaya vizuri ni sekta ya Utalii yenye miradi 191 ambayo ni asilimia 9.45 na sekta ya Tano kwa kufanya vizuri katika kipindi cha awamu ya sita ni sekta ya Kilimo yenye miradi 180 ambayo ni asilimia 8.91.

Kuhusu miradi Bw. Teri amesema katika kipindi cha Januari 2021 hadi Januari, 2025 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili jumla ya miradi 113 ukilinganisha na kipindi kama hicho cha Januari 2017 hadi Januari 10, 2021 ni mradi mitatu tu ya upanuzi ilisajiliwa.

"Ongezeko la usajili wa miradi ya upanuzi umetokana na mabadiliko katika Sheria mpya ya Uwekezaji ya mwaka 2022 iliyotoa unafuu wa vivutio vya uwekezaji kwa miradi ya upanuzi ambapo hapo awali ilikuwa haipati vivutio vya uwekezaji hasa vya kikodi. Lakini pia ongezeko husika linatokana na imani wawekezaji waliyonayo juu ya serikali katika masuala ya mazingira rafiki ya uwekezaji nchini, "

Na kuongeza kuwa" Matarajio ya Kituo cha Uwekezaji kwa mwaka wa 2025, yaliyowekwa katika Mpango Mkakati wake uliozinduliwa hivi karibuni ni kuwa Kwanza, kituo kina lengo la kusajili miradi elfu moja mia tano (1500) ya uwekezaji, katika kipindi cha msimu wa 2025 na kuweka malengo ya kuvutia mitaji ya kigeni yenye thamani ya bilioni 15, "ameeleza Bw. Teri

TIC imejipanga kuhakikisha kwamba, angalau asilimia kumi ya miradi iliyosajiliwa inalenga katika kuchangia juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuonyesha jitihada za kituo hicho za kusukuma mbele uwekezaji wenye manufaa na endelevu.



No comments:

Post a Comment