UZALENDO NI MSINGI WA MAENDELEO YA JAMII. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, February 25, 2025

UZALENDO NI MSINGI WA MAENDELEO YA JAMII.



Na WMJJWM -Morogoro


Imebainika kuwa ukosefu wa uzalendo miongoni mwa wananchi unachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa miundombinu na kuthamini miradi ya Maendeleo katika maeneo yao.

Hayo yamebanishwa Februari 25, 2025 wakati wa uwasilishaji wa mada ya uzalendo katika mafunzo ya mpango kazi wa Taifa wa kuhamasisha na kusimamia Maendeleo ngazi ya Msingi 2022/2023 - 2025/2026 kwa wawezeshaji ngazi ya Mkoa.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofanyika Mkoani Morogoro, yamewahusisha Maafisa Maendeleo wa Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii na Maafisa Mipango kutoka Mkoa wa Lindi, Tanga, Manyara, Mara, Pwani, Mtwara, Rukwa, Singida Arusha na Kilimanjaro.

Lengo la mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ni kuwajengea uwezo maafisa hao ili kutoa elimu ya uzalendo, ulinzi na utunzaji wa rasilimali na tunu za Taifa.

Akiwakilisha mada ya uzalendo na Afisa Maendeleo ya Jamii Alistedes Kalulu amesema kuna haja ya kufufua dhana ya uzalendo kwa maslahi ya kizazi cha sasa na baadaye ili kulinda rasilimali za nchi na Ustawi wa Maendeleo ya Jamii.

"Moyo wa uzalendo ni muhimu sana katika ujenzi wa Taifa imara, historia mila na desturi za taifa lolote duniani vinahitaji kuenziwa kuendelezwa na kurithishwa ili kulinda tunu za nchi kwa maslahi ya jamii nzima" amesema Kalulu.

Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Zukra Magachi amewataka maafisa hao kupeleka elimu waliyoipata ngazi ya Mtaa/ Kijiji ili kusaidia kueneza dhana ya uzalendo kwa wananchi na kuwafanya kuthamini na kulinda miradi ya kimaendeleo katika maeneo yao.

Kwa upande wake Afisa Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa James Kimambo amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo wawezeshaji katika kubadilisha mtazamo kwa wananchi kutambua kuwa maendeleo ni kwa ajili yao na hivyo kutunza na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miradi ya maendeleo.










No comments:

Post a Comment