WANAFUNZI WAKIKE WAHAMASISHWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 14, 2025

WANAFUNZI WAKIKE WAHAMASISHWA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI


Wanafunzi wa kike nchini wametakiwa kusoma masomo ya sayansi ili kuongeza idadi ya wanasayansi wa kike ambao watasaidia kuleta mageuzi ya sayansi na teknolojia.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wanawake katika Kazi za Barabara, Mhandisi Gladness Kitaly alipoambatana na ujumbe kutoka Wizara ya Ujenzi kutembelea Shule ya Sekondari Chamwino na kuelezea fursa zilizopo katika sekta ya Ujenzi.

“Tulikuwa tunaongea na Wanafunzi kuwahamasisha kutumia fursa ambazo Serikali imewawekea ili kuweza kujiinua kiuchumi kama Wahandisi na Wakandarasi, na kuwa kama Wajasiriamali katika sekta ya Ujenzi”, amesema Mhandisi Kitale.

Amemshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi, Aisha Amour kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wanawake washiriki katika zabuni za Ujenzi wa miradi ya miundombinu kuanzia ngazi ya chini hadi juu kwa Wanawake Makandarasi.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Chamwino, Adam Mtani ameipongeza Wizara ya Ujenzi kwa kuwatembelea na kuwaomba waendeleze juhudi za kuhamasisha Wanafunzi wa kike kusoma masomo ya Sayansi ili kuzalisha Wanawake wengi kwenye masuala ya Sayansi na teknolojia.

“Tumeweza kufaidika sana na ujio wenu, watoto wetu wa kike wamekuwa viongozi wazuri sana Darasani, mathalani mwaka 2024 watoto wakike wa nne wameweza kupata Daraja la kwanza”, amesema Mtani.

Naye, Mwanafunzi wa kike wa Shule hiyo Marta Magige ameishukuru Wizara ya Ujenzi kwa kusaidia na kusisitiza umuhimu wa masomo ya Sayansi ambayo ni chachu ya mabadiliko ya kimaendeleo katika Taifa.







No comments:

Post a Comment