WANANCHI WASHIRIKIANA NA POLISI KUJENGA KITUO CHA POLISI KIJIJI CHA MLONGIA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, February 19, 2025

WANANCHI WASHIRIKIANA NA POLISI KUJENGA KITUO CHA POLISI KIJIJI CHA MLONGIA.


Zaidi ya wanakijiji elfu mbili kutoka kijiji cha Mlogia, wilayani Chemba, wamekusanyika kushuhudia utekelezaji wa changamoto zao za ulinzi na usalama kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (SACP), George Katabazi.

Wananchi hao walikuwa wameomba kuongezewa Polisi kata na kupatiwa pikipiki kwa ajili ya kuwafikia haraka ili kuongeza ufanisi katika ulinzi na kujengewe kituo cha Polisi.

Kamanda Katabazi aliahidi kutatua changamoto zao na baada ya siku chache kupita baada ya kikao hicho Februari 18, 2025 amekabidhi pikipiki na kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kijiji cha Mlongia na kuendesha harambee ya ujenzi wa Kituo cha Polisi

Aidha, Katabazi amekabidhi pikipiki,na kuwaongezea Polisi kata katika Kijiji hicho pamoja na kutoa mifuko 20 ya Saruji na kuendesha harambee ya ujenzi wa Kituo hicho ambapo wananchi wameonyesha kuguswa na jambo hilo na kuchangia kiasi cha zaidi ya shilingi laki sita na mchanga wa ujenzi huo.

Katika hatua, nyingine wanakijiji wa Mlongia wamepongeza Jeshi la Polisi kwa kuwachukulia hatua stahiki wahalifu waliokuwa wakiwasumbua wanawake na kuahidi kumuunga mkono kamanda Katabazi katika kuhakisha wananchi hao wanapata kituo cha Polisi kupitia nguvu ya wananchi ili kuepukana na adha ya kutembea mda mrefu kupata huduma ya Polisi.





No comments:

Post a Comment