Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Imeelezwa kuwa kwa mara kwanza katika Historia ya Tanzania Serikali imetenga Shilingi Bilioni 6.3 kwaajili ya miradi ya Utafiti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi wakati milioni 600 zikielekezwa katika miradi ya usalama wa chakula.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu katika mkutano wake na Wanahabari akielezea mafanikio ya Taasisi hiyo kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan.
Ambapo ameongeza kuwa kupitia mfumo wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Serikali ya Tanzania na nchi rafiki pamoja na Taasisi za Kimataifa Taasisi hiyo imepokea Shilingi Bilioni 5.65 kwaajili ya utekelezaji miradi ya utafiti wa pamoja kati ya Watafiti wa Tanzania na washirika wake.
"Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Serikali imetenga Shilingi Bilioni 6.3 kwaajili ya miradi ya utafiti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,huku shilingi milioni 600 zikielekezwa katika miradi minne ya usalama wa chakula".
"Serikali ya awamu ya sita imetoa fedha na kuweka mazingira rafiki kwa wanasayansi na wabunifu wa Kitanzania. Kupitia mfumo wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Serikali ya Tanzania na nchi rafiki pamoja na Taasisi za Kimataifa, COSTECH imepokea shilingi bilioni 5.65 kwaajili kutekeleza miradi ya utafiti wa pamoja kati ya watafiti wa Tanzania na Washirika wetu".
Aidha ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan (2021-2025), Tanzania imeendelea kupiga hatua katika maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu. Kwa utashi thabiti wa kisiasa na dira ya kuifanya Tanzania kuwa taifa linalojegwa kwa kutumia sayansi na teknolojia.
Aidha Serikali imewekeza shilingi bilioni 25.7 katika utafiti, ubunifu na maendeleo ya teknolojia kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ambapo Serikali kupitia taasisi hiyo imefadhili zaidi ya tafiti 50 katika sekta za Elimu, kilimo, afya, na mazingira ili kuhakikisha maarifa haya yanatumika kuboresha maisha ya Watanzania.
''Hatua hii si tu kwamba imeendelea kuimarisha msingi wa maendeleo ya kisayansi, bali pia imethibitisha dhamira ya serikali ya kujenga taifa linalowekeza katika kuibua teknolojia, likiongozwa na tafiti na ubunifu''.
Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo amesema, Serikali kupitia COSTEC pia imefadhili zaidi ya vituo vya ubunifu 111 zimeimarishwa, huku tafiti zikibadilika kuuhisho za kisayansi kwa jamii.
''Kampuni mpya zipatazo 70 zimesajiliwa ikiwa na matokea ya wabunifu waliyowezeshwa na serikali yetu".
No comments:
Post a Comment