Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imewataka wananchi na wateja wake kuacha tabia ya kujiunganishia maji kinyume cha taratibu na kuingilia miundombinu ya maji.
Hayo yamebainishwa leo Machi 10, 2025 na Afisa Mapato wa DUWASA, Bw. Khalifa Ismaily wakati wa zoezi la ukaguzi wa miundombinu ya maji ili kubaini wanaohujumu miundombinu hiyo.
Amesema wakati wa zoezi hilo, DUWASA imembaini Bw. Mangendi Kisarazo, Mkazi wa Kisasa ambaye amejiungananishia miundombinu ya maji kinyume cha utaratibu.
“Wateja waache tabia ya kujiunganishia huduma ya maji kinyemela kwani sio sawa na haikubaliki ni vema wakafuata taratibu na kulipia maji kihalali, kwani DUWASA tukikubaini hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mteja yeyote yule” amesema Bw. Ismail
Kwa upande wake Bw. Mangendi Kisarazo, amekiri kuhusika kuhujumu miundombinu ya majisafi kwa kujiunganishia maji na kufanya shughuli zake na ameahidi kubadilika na kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment