KAMATI YA BUNGE YAIKUBALI RANDAMA YA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA YA MAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 26, 2025

KAMATI YA BUNGE YAIKUBALI RANDAMA YA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA YA MAJI


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeridhia na kuikubali randama ya mpango na bajeti ya Wizara ya Maji ya 2025/2026 katika kikao Bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) amesema vipaumbele katika bajeti hiyo ni pamoja na
Kuimarisha uwezo wa Wizara na Taasisi zake katika kutekeleza majukumu na 
Kufanya upembuzi yakinifu wa miradi mikubwa ya maji itakayotumia vyanzo vya uhakika vya maji.

 Miradi ya kimkakati itakayoendelea kutekelezwa ni pamoja na mradi wa maji wa Miji 28,Kuendelea na ujenzi wa Bwawa la Kidunda na mradi wa Jiji la Mbeya kwa kutumia chanzo cha mto Kiwira na kuendelea na utekelezaji wa mradi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika Mkoa wa Simiyu 

 Kukamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi wa kutoa maji ziwa Victoria kwenda katika mji wa Singida na Jiji la Dodoma.

Kamati ya Bunge ya Maji na Mazingira imeridhia na kuikubali randama ya Mpango na Bajeti ya jumla ya Shilingi 1,016,894,958,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Maji mwaka 2025/26 kwama ilivyo wasilishwa.

No comments:

Post a Comment