MAVUNDE ATOA MSAADA WA MADAFTARI 10,000 KWA WATOTO YATIMA NA WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 19, 2025

MAVUNDE ATOA MSAADA WA MADAFTARI 10,000 KWA WATOTO YATIMA NA WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU



Na Okuly Julius, Dodoma.


MBUNGE wa Dodoma mjini ambaye ni Waziri wa madini Mhe.Anthony mavunde ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya masomo kwa wanafunzi yatima na waishio maisha magumu wa shule zote za msingi zilizopo Dodoma jiji ili viwasaidie katika masomo yao.

Msaada huo ameutoa leo Machi 19, 2025 katika shule ya msingi Mazengo wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa vya masomo kwa watoto yatima na waishio mazingira magumu wa shule za msingi zote Dodoma jiji ambapo amekabidhi madaftari 10,000 na mabegi.

Mavunde amesema nia yake nikuona wanafunzi waishio mazingira magumu pamoja na yatima wanapata Elimu bora na kuwa na vifaa vyote vya kujifunzia sawa na wanafunzi wengine wenye uwezo .


" Kwa niaba ya shule zote zilizopo Dodoma jiji ninamkabidhi mkuu wa kamisheni wa Elimu za msingi Dodoma madaftari 10,000 ambayo yanakwenda kugawiwa kwa watoto yatima na watoto waishio mazingira magumu.

"Kipaumbele changu kikubwa kama mbunge wa Dodoma Mjini ni katika suala la Elimu,katika sekta ya Elimu tunazidi kuboresha ili watoto wetu wazidi kusomea katika mazingira bora na kwa wale wanao nifuatilia toka zamani na kunijua vizuri wanaelewa namna gani nimekuwa nikiipa Elimu kipau mbele sifanyi haya kwa kuhitaji kura kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi misaada hii naitoaga toka zamani na ukiangalia niliyowapa misaada hii ni watoto yatima ambao hawana wazazi kwa hiyo hawana wa kumshawishi anipigie kura",amesema Mavunde.

Akijibu yale yaliyowasilishwa katika risala na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mazengo Mwl.Rehema wakihitaji kujengewa uzio wa shule hiyo ili kutenganisha mipaka ya shule na makazi ya wananchi ,Mhe. Mavunde ameahidi kuwa atashirikiana na wanafunzi wote waliyohitimu katika shule ya msingi Mazengo kujenga uzio wa shule hiyo pamoja na kuwajengea uwanja wa michezo na kufanya ukarabati wa shule hiyo.

Pia ameongeza kuwa atachangia matofali 5,000 kwa ajili ya uwanzishaji wa ujenzi wa uzio huo huku akisema kuwa serikali itashirikishwa mara baada ya wao kuonesha juhudi zao binafsi.

"Nimemwambia mwalimu mkuu aende idara ya mipango awalete wataalamu waoneshe mipaka ya shule ili tuweze kuanza ujenzi wa fensi,na mimi katika hili nitajitolea matofali 5,000 pamoja na kuhakikisha nawahamashisha wale wote waliyo hitimu shule hii ili tushirikiane kujenga fensi hii,pia mmeomba suala la viwanja vya michezo mwezi ujao nitawajengea uwanja wa netball na wiki hii ntawawekea goli za vyuma na nyavu zake katika uwanja wa mpira wa miguu",amesema.

Akisoma lisara mbele ya mgeni rasmi Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwl.Rehema amesema shule ya msingi mazengo inajumla ya wanafunzi 8009 ambapo wavulani ni 390 na wasichana ni 419 huku walimu wakiwa ni 25 kati yao wakike ni 21na wakiume 3.








No comments:

Post a Comment