MBUNGE ELIBARIKI KINGU AKABIDHI PIKIPIKI 6 KWA UVCCM MKOA WA SINGIDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 25, 2025

MBUNGE ELIBARIKI KINGU AKABIDHI PIKIPIKI 6 KWA UVCCM MKOA WA SINGIDA



Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, amekabidhi pikipiki 6 kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida. Pikipiki hizo zimetolewa kwa ajili ya makatibu wa UVCCM katika wilaya zote sita za mkoa huo.

Mbali na hilo, Kingu ametoa bati 120 zenye thamani ya Shilingi Milioni 3.1 kwa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Singida pamoja na tiles zenye thamani ya Shilingi Milioni 7 kwa ajili ya ofisi ya CCM Wilaya ya Ikungi. Vilevile, ametoa Shilingi Milioni 3 kwa jumuiya za Wilaya ya Ikungi.

Hafla hiyo imefanyika leo Machi 24, 2025, katika Ukumbi wa RC Mission mkoani Singida, ambapo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Kawaida, alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa miradi ya kiuchumi ya UVCCM mkoani humo. Miradi hiyo ni vibanda vya biashara 73 na kampasi ya elimu ya kati ya Chuo cha St. Joseph.

Katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, alikabidhi gari kwa UVCCM Mkoa wa Singida.


KINGU: "NIMETIMIZA AHADI YANGU KWA VIJANA"

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mbunge Kingu alisema:

"Niliwaahidi vijana kuwa mkishikamana na mimi, kwa kidogo ninachokipata Bungeni, nitarudisha heshima kwa chama changu. Nilikuomba Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, wakati nikiwa Uingereza, uniruhusu nikamilishe ziara na nikabidhi hizi pikipiki mwenyewe. Leo nimetekeleza."

Mbunge huyo pia aliwasilisha risiti ya ununuzi wa pikipiki hizo kwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, akifafanua kuwa pikipiki hizo zimenunuliwa kwa jumla ya Shilingi Milioni 16.2, zimesajiliwa kwa TIN ya UVCCM na zimeshalipiwa kodi zote.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali, pamoja na wanachama wa UVCCM kutoka wilaya zote za Mkoa wa Singida.







No comments:

Post a Comment