WMA YAFANIKIWA KUHAKIKI ASILIMIA 94 YA VIPIMO, YATAJA CHANGAMOTO NA MIKAKATI YAKE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 25, 2025

WMA YAFANIKIWA KUHAKIKI ASILIMIA 94 YA VIPIMO, YATAJA CHANGAMOTO NA MIKAKATI YAKE



Na Okuly Julius_ DODOMA


Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Alban Kihulla, amesema wamefanikiwa kuhakiki asilimia 94 ya vipimo vilivyopangwa kuhakikiwa kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ameyasema hayo leo Machi 25,2025 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita

"jumla ya vipimo 3,668,149 kati ya vipimo 3,923,652 vilivyopangwa kuhakikiwa vilifanyiwa uhakiki, huku vipimo 102,969 vikiwa na mapungufu yaliyorekebishwa na kuruhusiwa kuendelea kutumika. Aidha, vipimo 5,607 vilibainika kuwa na mapungufu yasiyorekebishika na hivyo kuzuiwa kutumika, "amesema Kihulla

Bw. Kihulla amesema Kipindi cha Miaka Minne WMA imefanikiwa kuajiri maafisa wapya 186 wa ukaguzi wa vipimo, jambo linaloongeza ufanisi katika uhakiki na ukaguzi wa vipimo kote nchini.

" Wakala imepata vifaa vya kisasa vya kuhakiki vipimo, ikiwa ni pamoja na mitambo ya kuhakiki vipima mwendo, mita za maji, na flow meters kwa mafuta na gesi,

Na kuongeza kuwa" Kupitia ukaguzi wa mara kwa mara, vipimo vingi vimehakikishwa kuwa sahihi, na hivyo kuimarisha uadilifu katika biashara na sekta nyingine zinazotegemea vipimo, " amesema Kihulla

Amesema pamoja na mafanikio haya, WMA imebainisha changamoto kadhaa zinazokwamisha utekelezaji wake kwa ufanisi ikiwemo upungufu wa Maafisa wa Ukaguzi: Licha ya ajira mpya, bado kuna uhaba wa watumishi katika baadhi ya mikoa, Uelewa Mdogo wa Umma Kuhusu Vipimo Sahihi: Wafanyabiashara na wananchi wengi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa vipimo sahihi, hali inayochochea udanganyifu katika biashara na Upungufu wa Vifaa vya Kisasa: Wakala bado inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa baadhi ya vifaa vya kisasa vya kuhakiki vipimo vikubwa vya viwandani na gesi.

WMA imeanisha Mikakati ya Kukabiliana na Changamoto kuwa ni pamoja na kuendelea kuajiri maafisa wa vipimo na kuwapa mafunzo ya mara kwa mara, kutoa elimu kwa umma na wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi.

Pamoja na kuimarisha ushirikiano na vyombo vya sheria kudhibiti vipimo bandia na udanganyifu wa Vipimo na kuwekeza zaidi katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kuhakiki vipimo.

Kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2021/22 hadi Februari, 2025, Wakala imechangia jumla ya TZS Bilioni 17.1.

"Kwa mwaka
2021/2022 tulichangia bilioni 4.2, Mwaka 2022/2023 bilioni 4.4,mwaka
2023/2024 bilioni
4.7, Hadi Februari, 2025 tumechangia bilioni
4.3

Aidha, kwa mwaka wa fedha 2024/25 Wakala inatarajia kuchangia kwenye mfuko Mkuu wa Serikali zaidi ya TZS Bilioni 7 ambapo kufikia Februari, 2025, Wakala imekwisha changia kiasi cha TZS Bilioni 3.8.

No comments:

Post a Comment