

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa (MNEC) katikati akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka (kushoto) na Kulia ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa (MNEC) kulia akizungumza na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa
(kushoto)

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa (MNEC) Kulia akiteta jambo na Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Kite Mfilinge(kushoto)
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Hamoud Jumaa( MNEC), amesema kuwa miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan imekuwa na mafanikio makubwa kwa Taifa na Wananchi wake.
Jumaa amesema mafanikio hayo yametokana na sera na mikakati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imekuwa ikilenga kuongeza ushirikiano na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Kauli hiyo ya Jumaa imekuja ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais Samia kwa kazi alizofanya katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake tangu aliporidhi kiti hicho kutoka kwa mtangulizi wake Hayyati John Pombe Magufuli (JPM) aliyefariki Machi 2021.
Jumaa amesema kwa maoni yake Rais Dkt. Samia amefanikiwa kutokana na kusimamia mambo makubwa manne ambayo kimsingi yamesaidia kuleta tija na faida kwa Watanzania na Taifa nzima kiujumla.
Jumaa, ametaja jambo la kwanza kuwa ni ushirikiano katika jamii, ambapo amesema Serikali imehamasisha ushirikiano wa jamii katika maamuzi yanayohusu maendeleo ya elimu,afya na miundombinu.
Amesema jambo hilo ,limewapa Wazazi na wanajamii nafasi ya kutoa maoni na kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao bila kushurutishwa wala kulazimishwa.
Amesema kuwa,katika hilo Rais Samia ametoa fursa kwa jamii kujitegemea kiuchumi ambapo imewasaidia wazazi, Wanawake na Vijana kujenga biashara ndogondogo na kuboresha hali ya maisha.
Jumaa ametaja jambo la nne kuwa ni Kukuza Maadili na Umoja wa Jamii ambapo Rais Samia ameanzisha program za elimu ya maadili na nidhamu ambazo kwa kiasi kikubwa zimejikita katika kuimarisha uhusiano na umoja katika jamii.
Amesema suala la maadili na umoja limewasaidia wazazi na watoto kuishi katika mazingira yenye heshima , ushirikiano na jamii.
Hatahivyo,Jumaa amesema kwa ujumla juhudi hizo zinaongeza ushawishi wa Jamii katika kufanya maamuzi muhimu na kuchangia katika maendeleo endelevu huku zikisaidia kujenga jamii yenye ustawi wa kijamii na uchumi.
No comments:
Post a Comment