TANZANIA KUWA MWENYEJI WA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA eLEARNING AFRIKA MEI 2025 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 29, 2025

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA eLEARNING AFRIKA MEI 2025



Na Okuly Julius _ DODOMA


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Perof.Adolf Mkenda amasema Tanzania itakuwa nchi mwenyeji wa kongamano la kimataifa la earning Afrika linalotarajiwa kufanyika Mei 07 hadi 09, 2025 katika kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.

Hayo ameyasema leo machi 29,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema kongamano hilo litakuwa mara yapili kufanyika nchini.

Amesema kongamano hilo linalenga kuleta kwa pamoja makundi mbalimbali kutoka zaidi ya nchi 65 za Afrika kwa ajili ya kujadili,kubadilishana uzoefu,kuhamasisha uwekezaji na kuazimia mipango ya pamoja ya kuchagiza matumizi ya Teknolojia za kidijitali katika sekta ya Elimu barani Afrika.

“kongamaono la 18 la elearning afrika litafanyika katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini dar es salaam kuanzia mei 07 hadi 09 mwaka huu,tangu kuasisiwa kwake mwaka 2005 kongamano hili lishafanyika nchi 17 ikiwemo Tanzania.

“Tanzania lilifanyika mwaka 2021 hivyo mwaka huu litakuwa linafanyika kwa mara ya pili,kongamano hili linalenga kuwakutanisha wadau zaidi ya 1500 kutoka zaidi ya 65 barani Afrika”,amesema.

Pia amesema makundi hayo ya wadau yatajumuisha watunga sera,watoa maamuzi,wataalamu wa Elimu,wataalamu wa Teknolojia,watafiti,wabunifu,wafanya biashara,wawekezaji na wadau wa maendeleo.

Aidha amesema kongamano hilo litajumuisha mkutano wa mawaziri zaidi ya 50 kutoka nchi 49 barani Afrika utakao kuwa na lengo la kuazimia mikakati ya pamoja na kuandaa nguvu kazi mahiri katika kubuni, kuzalisha,na kuimalisha matumizi ya kidigitali.

“kama wenyeji wa kongamano hili nchi yetu inatarajia kunufaika na fursa mbalimbali kutokana na kuwa mwenyeji wa kongamano hili ambapo tutabaini mikakati mpya hususani katika sekta ya Elimu”,amesema.

Kongamano hilo litaenda sambamba na kaulimbiu isemayo “kufikilia upya Elimu,na maendeleo ya raslimali watu kwa ustawi wa Afrika”




No comments:

Post a Comment