TARURA KUUNGANISHA KATA YA GALAPO NA MAMIRE, BABATI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, March 3, 2025

TARURA KUUNGANISHA KATA YA GALAPO NA MAMIRE, BABATI


Babati, Manyara


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE imeondoa vikwazo na kuboresha miundombinu katika Halmashauri ya Mji wa Babati mkoani Manyara. 

Akizungumza katika mahojiano maalum, msimamizi wa mradi kutoka TARURA wilayani Babati, Mhandisi Naftal Lytuu amesema kwa mwaka wa fedha 2023/24 wilaya ya Babati ilipokea fedha kwaajili ya utekelezaji wa mradi wa uondoaji vikwazo katika barabara ya Mamire-Qash yenye urefu wa Km 26 na ujenzi wa makalavati 4 inayounganisha kata ya Galapo na Mamire.

Naye, Mwenyekiti wa kijiji cha Galapo, Bw. Said Juma ameeleza kuwa barabara hiyo itawasaidia wananchi kiuchumi.

“Barabara hii inaunganisha kata ya Endakiso, Galapo na Mamire barabara hii inasaidia sana katika kusafirisha mazao yetu, wagonjwa na shughuli za kila siku, ilikuwa kutoka huko ukifika hapa unafaulisha mzigo kwenye gari nyingine ila kwa sasa hata bei ya usafishaji itapungua“, amesema.

Naye, Bw. Nuru Ally mkazi wa kijiji cha Kayamangu ameishukuru serikali kupitia barabara hiyo imesaidia katika shughuli za usafiri kwasasa nauli ya pikipiki imepungua kwenda mjini, hivyo wanasafirisha mazao kwa bei nafuu.

"Barabara hii inamchango mkubwa kiuchumi inaunganisha kata 3 na barabara inayoelekea hadi wilaya ya Kondoa hivyo kurahisisha shughuli za usafishaji wa mazao na usafiri kutoka eneo moja kwenda jingine".

No comments:

Post a Comment