Viongozi wa Ulaya waunga mkono mpango wa nchi za kiarabu kuijenga upya Gaza - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, March 9, 2025

Viongozi wa Ulaya waunga mkono mpango wa nchi za kiarabu kuijenga upya Gaza


Mataifa makuu ya Ulaya yameunga mkono mpango unaoongozwa na nchi za kiarabu wa kuijenga Gaza upya kwa gharama ya dola bilioni 53 na kuepuka Wapalestina kuachwa bila ya makaazi katika eneo hilo.


Mpango huo ulioratibiwa na Misri na kuidhinishwa na viongozi wa nchi za kiarabu umepingwa na Israel na rais wa Marekani Donald Trump, ambaye amewasilisha mpango wake wa kuigeuza Gaza kuwa "eneo la kivutio mashariki ya kati".


Siku ya Jumamosi mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uingereza waliukaribisha mpango huo unaobaini kuwa ni "uhalisia" Gaza kujengwa katika miaka mitano.


Katika taarifa, wamesema mpango hupo umeahidi "maboresho ya haraka na endelevu kwa hali mbaya ya maisha" kwa watu wa Gaza.


Mpango huo unapendekeza Gaza iongozwe kwa muda wa mpito na kamati huru ya wataalamu na walinda amani wa kimataifa watumwe katika eneo hilo. Kamati hiyo itahusika kusimamia misaada ya kibinaadamu na masuala ya Gaza chini ya usimamizo wa mamlaka ya Palestina.


Pendekezo la mpango huo limezusha wasiwasi kuwa makubaliano hafifu ya kusitisha mapigano Gaza huenda yakavunjika baada ya kipindi cha wiki sita cha awamu ya kwanza ya makubaliano hayo kumalizika Macho mosi.


Israel imesitisha misaada kuingia katika eneo hilo kuishinikiza Hamas kukubali mpango mpya wa Marekani wa kuongeza muda wa makubaliano hayo ya kusitisha mapigano, wakati ambapo mateka wanaozuiwa Gaza wataachiwa ili kwa upande mwingine wafungwa wa Palestina nao waachiwe huru.


Lakini Hamas inasisitiza kuwa awamu ya pili ya makubaliano hayo, ambayo itashuhudia kuondoka kikamilifu kwa vikosi vya Isreali, inastahili kuanza kama ilivyokubaliwa.


Israeli itatuma kundi la kufanya majadilianoQatar Jumatatu kushiriki katika mazungumzo ya kuongeza muda makubaliano hayo ya kusitisha mapigano, ofisi ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu imesema.


Haijabainika lini na iwapo awamu ya pili ya makubaliano hayo ya kusitisha mapigano itatekelezwa.

No comments:

Post a Comment