Wakazi Pugu Stesheni waipongeza wizara mradi wa maji kusini mwa Dar - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 18, 2025

Wakazi Pugu Stesheni waipongeza wizara mradi wa maji kusini mwa Dar


Wakazi wa kata ya Pugu Stesheni Jijini Dar es Salaam wameipongeza Wizara ya Maji kwa kuimarisha huduma ya maji maeneo hayo.

Pongezi hizo wamezitoa leo wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ambaye ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya maji kusini mwa Dar es Salaam ambao umeanza kufanyiwa majaribio ya kutoa huduma.

Amina Juma pamoja na Latifa Singano wakazi wa eneo la Kifuru wamesema changamoto ya huduma ya maji katika maeneo yao ilikuwa kubwa hali ambayo ilisababisha shughuli nyingine za kiuchumi kukwama. Wamempongeza Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kwa mradi huo ambao umegharimu shilingi Bilioni 36.8.

Naye Diwani wa Kata hiyo Mhe. Shaban Musa Maulid amesema malalamiko makubwa kwa kata hiyo ilikuwa ni maji. Kukamilika kwa mradi huo kumeondoa malalamiko na kuwafanya wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Mhe. Aweso amewahakikishia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza changamoto zote za mradi zipatiwe ufumbuzi na wananchi waunganishiwe huduma ndani ya siku saba mara tu wanapokamilisha taratibu za maombi. Aidha, bili za huduma ya maji ziwe halisia.

No comments:

Post a Comment