Na WMJJWM,Dodoma.
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Faithmary Lukindo amewataka wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana kuwapa watoto fursa za michezo, uchangamshi kwa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni na Mila za Kitanzania katika uendeshaji wa vituo hivyo kwa lengo la kuhakikisha watoto wanafikia utimilifu wao na kupata jamii ya watu wenye maadili na nidhamu.
FaithMary ameyabainisha hayo leo Machi 01,2025,Jijini Dodoma wakati anazungumza na wamiliki wa vituo vya kulelea watoto mchana(Day Care centers) chenye lengo la kupata uongozi wa mpito wa kitaifa wa umoja huo.
Amesema wamiliki wa vituo vya kulelea watoto mchana wana jukumu la kipekee la kuhakiksha watoto wanapata fursa za kucheza michezo mbalimbali, kupata lishe bora wawapo vituoni ,nidhamu na kusimamia vema wasimamizi na walezi wa watoto vituoni.
“Familia zina jukumu la msingi la kuhakikisha watoto wanalelewa vyema na kuwa na maadili mema lakini wanapokua katika vituo vya kulelela watoto wadogo mchana ni jukumu lenu kuwasimamia walezi hao wanawafundisha watoto katika muktadha unaozingatia mila na tamaduni za kitanzania”Amesema Faithmary.
Naye Kaimu mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii kutoka OR-Tamisemi,Haroun Haroun amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wamiliki wa vituo hivyo katika ngazi za halmashauri na mikoa hivyo wamiliki hao wawiwe kutoa huduma kwa watoto kwa kuzingatia taratibu na kanuni zilizowekwa katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa linalohusika na masuala ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Mtoto (children in Crossfire )Craig Ferla amewakumbusha wamiliki hao kuwekeza jitihada nyingi katika kujenga utimilifu wa ubongo wa watoto na kuiahidi serikali kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha.
Viongozi wa mpito wa umoja huo waliopatikana kwenye uchaguzi ni Mwenyekiti(Shukuru Mwakasege)
Makamu mwenyekiti(Linner Roman)
Katibu(Mkambala Idd)
Katibu msaidizi( Salome Isack)
Mweka hazina(Patrick Msuta)
Baada ya katiba kupatikana na usajili wa umoja huo kukamilika,Viongozi wapya watachaguliwa.
No comments:
Post a Comment