Na Okuly Julius _ DODOMA
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umesema kuwa kupitia mradi wa minara 758 itawafikia wanachi milioni 8.5 katika mikoa 26 ya Tanzania Bara kwa gharama ya shilingi bilioni 126.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Taasisi hiyo leo Machi 27,2025 jijini Dodoma, Mtendaji Mkuu wa UCSAF Mhandisi Peter Mwasalyanda amesema kupitia Mradi huo vijiji 1407,Kata 713,wilaya 127 katika mikoa 26 zitanufaika na mpaka sasa minara 430 Sawa na asilimia 57 imeshajengwa kati ya 758.
"Pamoja na mradi huo pia tumeboresha minara 304 kuiongezea nguvu kutoka kwenye 2G hadi 3G kwa gharama ya zaidi ya bilioni 5,"
Na kuongeza kuwa "Dhamira ya serikali ni kuona wanachi hawapati changamoto ya Mawasiliano kwani bila Mawasiliano mazuri hata suala la ukuaji wa uchumi utakuwa mdogo kwani biashara nyingi kwa sasa zinategemea mtandao madhubuti hivyo jitihada hizi za kuboresha Mawasiliano nchini zinalenga kuchochea maendeleo, "amesema Mhandisi Mwasalyanda
Katika kukuza TEHAMA shuleni UCSAF kwa kushirikiana na DIT, UDOM na Must wametoa mafunzo kwa Walimu 3,798 katika shule 1791 ambapo Zanzibar Walimu ni 326 na Tanzania Bara Walimu 3,180.
" Katika kipindi cha miaka minne ya Awamu ya Sita Walimu 1,585 Wamepata mafunzo ya TEHAMA na lengo ni kuwajengea uwezo walimu kutatua matatizo ya vifaa hivyo,"ameeleza Mhandisi Mwasalyanda
Mhandisi Mwasalyanda amesema Shule 1,121 zimefikishiwa vifaa vya TEHAMA kwa Wastani shule hupata Kompyuta 5, Printa moja na Projecta moja ambapo Gharama za mradi ni shilingi Bilioni 5.94
"Katika kipindi cha miaka minne ya Awamu ya sita shule 469 zimepelekewa vifaa vya TEHAMA
Lengo ni kukuza ujuzi wa TEHAMA kwa Wanafunzi na Walimu nchini," amesema Mhandisi Mwasalyanda
KUTOA VIFAA VYA TEHAMA KWA AJILI YA KUBORESHA HUDUMA ZA POSTA
Mhandisi Mwasalyanda amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, inatambua umuhimu wa shirika la Posta nchini na hivyo katika kipindi cha miaka minne Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imekuwa ikiliwezesha shirika la Posta kwa kulipatia vifaa vya TEHAMA ili shirika liweze kutoa huduma kidigitali.
Ambapo tarehe 12 Julai 2024, UCSAF ilinunua PDA 250 na kuwakabidhi Shirika la Posta. Gharama za utekelezaji wa mradi huu ni kiasi cha TZS 161,926,471/=.
Mwezi Aprili 2025, UCSAF itakabidhi vifaa vingine 250 kwa shirika la Posta vyenye thamani ya TZS 161,926,471/=
No comments:
Post a Comment