WANAWAKE ACHANENI NA KAUSHA DAMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, March 3, 2025

WANAWAKE ACHANENI NA KAUSHA DAMU


Serikali imewapatia mitaji wanawake kwa ajili ya kuongeza kipato na kujikwamua na umaskini ikiwemo mifuko ya uwezeshaji wanawake kiuchumi hivyo ni wakati wa kuachana na vikundi vya mikopo isiyo fuata taratibu, maarufu kausha kama damu.

Spika Wabunge Mstaafu Mhe. Anna Makinda ameyasema hayo katika kongamano kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8.

Kongamano limewakutanisha wanawake kutoka mikoa ya Singida,Iringa na Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mhe Makinda amesema Wanawake lazima waamke na kupambana kwani Idadi ya wanawake waliopo katika uongozi imeongezeka huku wakishika nyadhifa mbalimbali ikidhihirisha kuwa hakuna kikwazo kwa mwanamke yoyote katika masuala ya uongozi 

Amesema hali hiyo imechagizwa kwa kiwango kikubwa kutokana na uongozi imara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza nafasi za uongozi na maamuzi kwa wanawake.

“Hakikisheni mnatumia vyema mikopo ya uwezeshaji na yenye gharama nafuu na mzingatie mikopo hiyo isiwe ya kukausha damu” 

Amesema ni muhimu kugeuka nyuma na kuwashika wanawake wengine ili kwa pamoja tuweze kuinuka na kwenda mbele.


Na upande wake Mkuu wa Mkuu wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule amesema kuwepo kwa wanaweke wenye nyadhifa kubwa katika serikali kunadhihirisha utashi wa nchi katika kuhakikisha usawa wa kijinsia .

Amesema ni wakati wa mwanamke kusimamia haki zake za msingi kwa kuwa kila kitu kimewekwa wazi kwa kutengeneza fursa nyingi zilizopo katika nyanja mbalimbali

Amesema itasaidia kupiga hatua moja kwenda nyingine kwa kujiongezea uwezo kwa nafasi zilizopo.

Maadhimisho hayo yameongozwa na kaulimbiu “wanawake na wasichana 2025 tuimarishe haki,usawa na uwekezaji"

No comments:

Post a Comment