Na Mwandishi Wetu, Arusha
Baadhi ya Watumishi Wanawake Wizara ya Madini Makao Makuu ni miongoni mwa wanaoshiriki Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani inavyofanyika kitaifa jijini Arusha.
Wakati huo, huo baadhi ya watumishi hao wanashiriki maadhimisho hayo jijini Dodoma.
Pamoja na Watumishi wa Wizara kushiriki jijini Arusha, pia taasisi zake ikiwemo ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ( GST), Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) pamoja na Vyama vya Wanawake katika Sekta ya Madini ikiwemo Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania ( TAWOMA) na TWIMMI) wanashiki pamoja na kuonesha shughuli mbalimbali katika mnyororo wa shughuli za madini.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kitaifa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu.
Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji"
No comments:
Post a Comment