
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akijadiliana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Bi. Helena McLeod mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo katika Jiji la Seoul Nchini Korea Kusini, Machi 13, 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Bi. Helena McLeod wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo katika Jiji la Seoul Nchini Korea Kusini, Machi 13, 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akibadilishana mawasiliano na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Bi. Helena McLeod mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo katika Jiji la Seoul Nchini Korea Kusini, Machi 13, 2025. Kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini Mhe. Balozi Togolani Mavura.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) akizungumza na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Bi. Helena McLeod Makao Makuu ya Taasisi hiyo katika Jiji la Seoul Nchini Korea Kusini, Machi 13, 2025. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini Mhe. Balozi Togolani Mavura, na kulia kwa Bi Helena ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) Prof. Eliakim Zahabu (wa kwanza upande wa kulia).
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Bi. Helena McLeod kuhusu Biashara ya Kaboni.
Mazungumzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo katika Jiji la Seoul Nchini Korea Kusini, Machi 13, 2025 ambapo Waziri Masauni yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi ambapo ameambatana na viongozi mbalimbali wa Ofisi ya Makamu wa Rais akiwemo Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi pamoja na Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) Prof. Eliakim Zahabu..
“Napongeza dhamira yako ya kufanya kazi bega kwa bega na nchi wanachama kuunga mkono na kukuza ukuaji wa uchumi endelevu na shirikishi kupitia ajenda ya ukuaji wa kijani. Ipasavyo, ziara yetu kwa GGGI leo iko ndani ya mfumo huo huo, tukizingatia maeneo yafuatayo.
Amesema kitu cha kwanza cha kujivunia ni uanzishwaji wa Kituo cha Kitaifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) ambacho kina jukumu la kufuatilia utoaji wa hewa ukaa nchini, hivyo ujuio wake nchini Korea Kusini ili kujifunza kuhusu kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji wa mikopo ya kaboni, usimamizi wake, uuzaji, na mbinu bora katika sekta nzima.
“Tuko katika hatua za mwisho za mchakato wa ndani na imani yetu kubwa kwamba wakati muafaka kwetu kujihusisha na kuona jinsi tunavyoweza kupata utaratibu uliopo wa kutusaidia kujenga uwezo wetu wa kubuni miradi inayofadhiliwa katika nyanja husika.”






No comments:
Post a Comment