ZAIDI YA WANANCHI 2000 KATA YA IHUMWA WANUSURIKA NA UHALIFU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 22, 2025

ZAIDI YA WANANCHI 2000 KATA YA IHUMWA WANUSURIKA NA UHALIFU.


Wananchi wa Kata ya Ihumwa Jijini Dodoma wameonyesha juhudi za kujitolea kujenga kituo cha polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kitakacho saidia kudhibiti matukio ya uhalifu pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa wahalifu hao.

Kauli hiyo imetolewa na wananchi hao March,22,2025 wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi akiungana na wadau wapenda maendeleo katika kata hiyo na kutoa vifaa vitakavyo saidia ukamilishwaji wa kituo hicho.

Aidha Katabazi ameendesha harambee kwa wananchi ya ukamilishwaji wa kituo hicho na kuchangia boksi 26 za vigae huku wananchi wakichangia milango na kupatikana kiasi cha fedha shilingi milioni mbili na laki tano Ts,2,500,000/=.

Vilevile Katabazi ameeleza mipango mikakati ya kuzuia na kutanzua uhalifu katika Jiji la Dodoma na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na kujenga imani kwa Jeshi hilo katika utoaji wa huduma.

Hata hivyo Uongozi wa kijiji pamoja na wananchi umepongeza Jitihada za Jeshi la Polisi za kuunga mkono ujenzi wa kituo hicho, kinachojengwa kwa nguvu ya wananchi huku wakieleza umuhimu wa uwepo kituo cha Polisi katika kata hiyo.

Kituo cha Polisi kata ya Ihumwa kilichopo wilaya ya kipolisi Mtumba kinatarajiwa kukamlishwa mwezi May,2025 na kusaidia zaidi ya wananchi 2000 wa kata hiyo.






No comments:

Post a Comment