Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa eneo la Kariakoo sio eneo la Siasa ni eneo la Biashara .
Chalamila ametoa kauli hiyo leo Aprili 22,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi habari kuhusu tukio la kukamatwa kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Heche na baadhi ya Wafuasi wa wafuasi wa Chama hicho katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
"Dar es Salaam hasa eneo la Kariakoo ni very Sensitive hivyo tunatumia nguvu kubwa kuhakikisha usalama wa watu na mali zao unakuwepo kwani kuna wafanyabiashara wengi sana sasa ukija tena kuongeza mkutano wa hadhara tena wa siasa unasababisha msongamano usio wa lazima,"ameeleza Chalamila
No comments:
Post a Comment