KATIMBA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KULIOMBEA TAIFA NA UCHAGUZI MKUU 2025 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 7, 2025

KATIMBA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KULIOMBEA TAIFA NA UCHAGUZI MKUU 2025



OR-TAMISEMI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Zainab Katimba amewaomba viongozi wa dini pamoja na waumini wa madhehebu yote nchini kuliombea Taifa na pia kuliombea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu 2025.

Mhe. Katimba ametoa ombi hilo alipomuwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

Ametoa msisitizo kwa Watanzania wote kuendelea kuilinda amani na utulivu wa nchi.

"Tunawaomba sana viongozi wa dini ya Kiislamu na madhehebu mengine, tuweke msisitizo mkubwa katika kuiombea nchi yetu. Ni jambo kubwa sana kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kuzingatia misingi ambayo tumejiwekea kwa miaka mingi."

"Tusifanye uchaguzi kuwa sababu ya kuchochea na kuleta mazingira yatakayoharibu amani ambayo nchi yetu imekuwa nayo kwa miaka mingi," amesisitiza.

Katika harambee hiyo, ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo Mbunge wa Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mhe. Hassan Bomboko, pamoja na Shekhr wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiasi cha Sh.Milioni 32.85 kilipatikana. Kati ya hizo, fedha taslimu zilikuwa Sh.milioni 7.75, michango kupitia benki sh.milioni 3.2, na ahadi ni sh.milioni 21.9.





No comments:

Post a Comment