MAFUNZO ELEKEZI KWA WAAJIRIWA WAPYA NI MUHIMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 28, 2025

MAFUNZO ELEKEZI KWA WAAJIRIWA WAPYA NI MUHIMU


Wizara ya Maji imeratibu mafunzo kwa watumishi wapya kwa kushirikiana na Chuo cha Utumishi wa Umma.

Mafunzo hayo yamehusisha waajiriwa wapya 60 na kufanyika mji wa Serikali jijini Dodoma.


Mafunzo yatadumu kwa siku tatu ambapo Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu Bi. Christina Akyoo akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waajiriwa wapya kuhusu misingi, Sheria, Kanuni ,Taratibu pamoja na Maadili ya utumishi wa umma .

Amesema mafunzo hayo ya awali ni utekekezaji wa takwa la kisheria kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma zitakazo wawezesha waajiriwa wapya kutambua misingi ya utoaji wa huduma bora kwa wateja ,elimu kuhusu rushwa na madhara yake mahala pakazi na utunzaji wa siri.

Mafunzo yanasisitiza kufanya kazi kwa upendo,ushirikiano na umoja kipindi chote cha utumishi wa umma, ikiwemo kufikia azma ya serikali ya kufikisha huduma ya maji kwa wananchi kwa asilimia 95 mIjini na 85 vijijini.

Kada zilizo shiriki mafunzo hayo ni pamoja na waandishi waendesha ofisi,wahandisi,madereva, na wataalamu wa ubora wa maji.

No comments:

Post a Comment