
Na Mwandishi Wetu ,Iringa
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) amewataka wafanyakazi wa Wakala huo kuwekeza nguvu katika kuwahudumia wananchi.
Ameyasema hayo leo tarehe 4 Aprili , 2025 wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TARURA linalofanyika katika ukumbi wa Masiti mkoani Iringa.
Mhandisi Seff amesema kwamba kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano italeta ufanisi na kuendelea kulinda taswira ya Wakala huo.
Hata hivyo Mtendaji Mkuu huyo ameahidi kusimamia yale yote yatakayoamuliwa katika mkutano huo na kuyafanyia kazi kwa ufanisi.
Naye, Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutoka TUGHE Bw. Mudathiri Ismail amewapongeza TARURA kwa namna walivyojipanga kutoa elimu hususan ya uwekezaji kwa wafanyakazi pia amewataka wajumbe kuishauri vizuri menejimenti ili TARURA izidi kusonga mbele kwani inawagusa wananchi moja kwa moja.
Wakati huohuo Mwakilishi wa Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Eunice Tesha ameipongeza TARURA kwa kujua dhana ya ushirikishwaji kwani mkutano huo ni fursa pekee ya kuwasilisha na kutoa maoni na kujadili kwa ustawi wa Wakala.










No comments:
Post a Comment