Mamia ya wananchi wa Zanzibar wamejitokeza kwa wingi kupata huduma za vipimo mbalimbali zinazotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kama sehemu ya kikao kazi cha 20 cha maafisa habari, mawasiliano na itifaki wa serikali kinachoendelea katika Viwanja vya Amaan, Zanzibar.
Huduma hizo, zilizoanza kutolewa jana tarehe 3 Aprili 2025, zinajumuisha upimaji wa macho, upimaji wa presha, vipimo na ushauri wa afya ya figo, tathmini ya afya ya akili, pamoja na ushauri wa lishe kutoka kwa wataalamu bingwa wa hospitali hiyo.
Huduma hizi, ambazo zinatolewa bila malipo kwa wananchi, zitapatikana hadi tarehe 7 Aprili 2025 zikilemga kutoa vipimo na ushauri wa huduma muhimu za afya kwa jamii, hasa kwa wale wanaokosa fursa ya kupata huduma za kibingwa katika maeneo yao.
Hizi hapa ni picha mbalimbali zikionyesha wananchi wakiwa katika banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiwa na shauku ya kupata huduma bila malipo na ushauri kutoka kwa wataalamu wa hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment