MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO AFARIKI DUNIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, April 13, 2025

MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO AFARIKI DUNIA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wamefariki dunia kwenye ajali ya gari wakiwa njiani kutoka mkoani Mwanza wakielekea wilayani Bunda Mkoa wa Mara.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo usiku wa kuamkia leo Aprili 13, 2025.


Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mara, Nickson Babu amesema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda.


Endelea kufuatilia OKULY BLOG , ambapo tutaendelea kukupatia taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment